Saturday, January 6, 2018

Ugua Pole Mh Lissu


Tunakuombea uzidi kuimarika kiafya na kila la kheri katika ngwe ya pili ya matibabu.

5 Januari 2018

Saturday, December 16, 2017

Uzinduzi wa Mradi wa Kinamama Mji Mpya



Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Mhe. John Mnyika akikata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua mradi wa akina mama wa Mtaa wa Mji mpya Jimbo la Kibamba.

Mradi huu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi  aliyoitoa Mhe. John Mnyika na Mwenyekiti wa Serikali ya  Mtaa Mhe. Aron Moye (kushoto kwa John Mnyika) wakati wakiomba ridhaa kwa wananchi.

Mhe John Mnyika na Mhe. Aron waliahidi kusaidia kuanzisha vikundi vya akinamama vya ujasiriamali.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya ufunguzi huo Mhe. John Mnyika aliwapongeza wakina mama hao kwa kuweza kutengeneza mfumo wa kusimamia mradi huo kabla haujaanza kwani miradi mingi imekufa kutokana na usimamizi.

Amewataka akina mama hao kuunganisha nguvu ya pamoja ili kufikia malengo waliojiwekea.

Akitoa majibu ya changamoto zilizowasilisha Mhe. Mnyika aliahidi kufatilia ujenzi wa daraja kutoka Mji Mpya kueleka barabara kuu kupitia kwa Mangi na kumuelekeza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kumpatia nakala ya maombi ya kupatiwa fedha kwaajili ya ujenzi huo aliyoiwasilisha Manispaa  kupitia kikao cha WDC ili kuweza  kuitengea fedha kwenye mfuko wa Jimbo.

Tuesday, December 5, 2017

Nasimama na Wabunge na Makamanda wetu waliokamatwa Morogoro




Nasimama na wabunge wetu wawili; Ndugu Peter Lijuakali na Susan Kiwanga, Madiwani wetu wawili na wanachama wetu 34 ambao kwa mara ya pili sasa bado wanakataliwa kupewa dhamana.
Ikumbukwe walikamatwa toka Novemba 26 mpaka sasa wananyimwa haki yao ya msingi ya kupata dhamana.
Ninaheshimu mhimili wa Mahakama; lakini kwa yaliyowahi kwisha tokea na mifano lukuki inasukuma hitaji la sauti zetu. Kumeshakuwa na njama ovu nyingi dhidi yetu wapinzani hasa ktk suala zima la utoaji wa haki ya msingi ya dhamana-inahitaji kupazwa sauti zetu na kuunganisha nguvu kukemea hili.
Tuungane ktk hili na madhila mengine mengi ya uvunjifu wa haki, demokrasia na usawa ktk kuendesha siasa nchini.
Tunahitaji siasa safi ili tuweze kupiga hatua kimaendeleo kama alivyotuasa Baba yetu, Mwl. Julius Nyerere

Thursday, August 3, 2017

MHE. JOHN MNYIKA AMTAKA RAIS ATEUE WAZIRI WA NISHATI NA MADINI KUONGOZA MAJADILIANO KUHUSU MADINI

MHE. JOHN MNYIKA AMTAKA RAIS ATEUE WAZIRI WA NISHATI NA MADINI KUONGOZA MAJADILIANO KUHUSU MADINI

Mbunge wa Jimbo la Kibamba, ambae ni Waziri kivuli wa nishati na madini, Mhe. John Mnyika, akiongea katika Mkutano wa hadhara Jana Jumatano 2/8/2017 eneo la Goba mwisho katika Jimbo la Kibamba, Mhe. Mnyika amemtaka Rais Magufuli ateue Waziri wa nishati na madini ili aongoze majadiliano kuhusu madini.

"Ni muda mrefu umepita Rais ajateua Waziri wa nishati na madini, ambae ndiye anayestahili kuongoza majadiliano kuhusu madini, badala yake anamuachia Waziri wa Katiba na Sheria kuongoza majadiliano kuhusu masuala ya madini, Ameamuachia Waziri wa Katiba na Sheria kwa sababu alikuwa kwenye tume ya mabadiliko ya Katiba, nae amekataa kuendeleza mabadiliko ya Katiba mpya" amesema Mnyika.

Amesema Serikali makini isingeanza na makinikia huku madini yanaendelea kuchimbwa na kutoka, wakati kuna makampuni mengine yanaendelea na uchimbaji, na kampuni inayoingoza kwa uzalishaji ni kampuni ya Geita Gold mine (GGM) na inaendelea na uchimbaji hakuna ufuatiliaji wala majadiliano yeyote yanayoendelea, huku Taifa likielekezwa kwenye majadiliano kuhusu makinikia badala yafanyike majadiliano kuhusu madini kwa upana wake.

 KATIBA MPYA

Mwaka 2010, akiwa Rais Kikwete, Mnyika ndiye aliyeibua mjadala kuhusu Katiba mpya ambapo ilipelekea hatua mpaka Rais Kikwete akaanzisha mchakato wa kipatikana Katiba mpya.

Mnyika ameahidi katika Bunge lijalo litakaloanza Septemba 5 mwaka huu kuanzisha tena mjadala mpya utakaopelekea kupatikana kwa Katiba mpya ambayo ndiyo suluhisho ya mambo mengi yanayoendelea.

KUHUSU MIRADI NA KERO JIMBONI
Katika mkutano huo wananchi walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali yanayohusu miradi na kero mbalimbali katika Jimbo, ambapo alisimama Mstahiki Meya wa Ubungo, Mhe. Boniface Jacob ambae alijibu maswali mbalimbali ya wananchi, pia kuwataka vijana na wakina mama kujitokeza kwa wingi kwani kuna mikopo ambayo inatolewa kwa ajili ya kufanya ujasiriamali na kujiendeleza katika mambo mbalimbali.

Na Sunday Urio
Katibu Msaidizi wa Mbunge, Jimbo la Kibamba

2 Agosti Mkutano wa Hadhara wa Mbunge: Goba Mwembe Madole








Monday, July 24, 2017

24 July: Ziara ya Ukaguzi wa Miradi katika Kata zote


Mbunge Wa jimbo la Kibamba Mh John John Mnyika leo tarehe 24/07/2017amefanya ziara ya kukagua miradi iliyofadhiliwa na Mfuko Wa Jimbo katika Kata zote sita zinazounda Ji mbo hilo ambazo ni Kata ya Saranga, Goba, Mbezi, Msigani, Kwembe na Kibamba.

Miradi hiyo ambayo ni vyoo vya Shule ya secondari Mpigimagohe , Kivuko cha Kibungobungo Kibamba, Ofisi ya Selikaliya mtaa Kinzudi Goba, Simtank Shule ya msingi msakuzi pamoja na fedha zilizoelekezwa kwenye vikundi vya ujasiliamali wanawake na vijana kwaajili ya kukuza mitaji yao.

Pia Mhe Mbunge aliwaagiza watumishi Wa Manispaa ya Ubungo kukamilisha miradi ambayo haijakamilika kwa wakati  ili kufikia malengo yaliyo kusudiwa  kupitia fedha za mfuko huo.